News

TANZIA YA PADRE GIANCARLO FRIGERIO

Published on October 09, 2026

Kwa masikitiko makubwa tunaomboleza kifo cha Padre Giancarlo Frigerio, aliyekuwa mwanashirika lwa Shirika la Watumishi wa Upendo (Don Guanella).  Kifo kilitokea tarehe 30/09/2026..

Padre Giancarlo alikuwa mwanashirika wa kwanza kuja kufanya utume kwenye jimbo letu. Alifanya utume kwenye parokia ya Iwindi. 

Tarehe 05/10/2026 tuliadhimisha misa ya kijimbo ya kumwombea apokelewe mbinguni. Misa ilifanyika pale kwenye parokia ya Iwindi. Tuendelee kumwombea apumzike kwa amani.

Asanteni.